Ulanguzi waendelea stand ya mabasi ubungo
imewekwa na admin
muda 2014-03-19 11:08:19
Watazamaji 2785
Ulanguzi waendelea stand ya mabasi ubungo
Uko hapa : Home > Habari kuu>

Dar es Salaam. Nauli za mabasi ya mikoani na nchi jirani zimeendelea kupanda, na sasa Mikoa ya Iringa na Tanga nayo imeguswa na ongezeko hilo.

Mbali na nauli hizo kuzidi kupanda, hali ya usafiri nayo imeendelea kuwa mbaya na kuleta usumbufu mkubwa wananchi kutokana na idadi ndogo ya mabasi katika Kituo Kikuu cha Ubungo (UBT).

Ongezeko la nauli katika Mikoa ya Iringa na Tanga hasa kwenye Wilaya ya Lushoto, lilibainika jana wakati maofisa wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) walipofanya ukaguzi UBT.

Mwananchi jana ilifika katika kituo hicho na kushuhudia idadi kubwa ya watu waliokuwa wakitafuta usafiri wa kwenda mikoani.

Wakizungumza kituoni hapo baadhi ya abiria walidai kuwa baada ya hali kuwa mbaya katika mikoa ya Kilimanjaro na Arusha, sasa imehamia Mikoa ya Iringa na Tanga.

Nauli za Arusha na Kilimanjaro zimepanda kufikia Sh35,000, Sh40,000 na Sh50,000 badala ya nauli ya kawaida ya Sh23,000 na 25,000 kwa mabasi ya kawaida.

Nauli ya Iringa nauli imepanda kutoka Sh18,000 na Sh20,000 hadi kufikia Sh40,000 na Sh50,000. Tanga imepanda kutoka Sh10,000 na Sh12,000 hadi kufikia Sh20,000.

Mmoja ya abiria aliyejitambulisha kwa jina la Subira Ramadhani aliyekuwa akisafiri kwenda Iringa, alisema nauli imefika Sh40,000 na Sh50,000 kutoka Sh18,000 na Sh20,000.

“Kama unavyoona, hapa hali ya usafiri ni mbaya magari hakuna, nauli ya kwenda Iringa imefika Sh50,000. Ni hatari kubwa kwa wasafiri,” alisema Ramadhani.

Ofisa kutoka Chama cha Kutetea Abiria (Chakua), Gelvas Rutabuzinda alikiri kuwa hali bado ni mbaya kutokana na baadhi ya mabasi kupandisha nauli.

“Kama unavyona bado hali siyo shwari, nauli zinaendelea kupanda abiria wanalubuniwa,” aliongeza Rutabuzinda.

Naye Ofisa Leseni wa Sumatra Sebasitian Lohay alisema mpaka sasa mabasi zaidi ya 20 yametozwa faini kwa makosa ya kupandisha nauli.

“Dhamira yetu ni kuona utaratibu na sheria zinafuatwa, watakaokiuka hatutasita kuwachukulia hatua zinazostahili na hata ikibidi kuwafutia leseni za usafiri,” alisema zaidi.

“Mpaka sasa tumeyakamata na kuyatoza faini zaidi ya mabasi 20 ya mikoani. Faini tulizowatoza ni kati ya Sh200,000 na 250,000 kwa makosa ya kupandisha nauli na bado tunaendelea na operesheni hii,” alisema Lohay.

Unasemaje kuhusu hii?

George g mlasani alisema, tarehe 2016-04-21 07:01:38:
Mabadiliko yeyote yanachangamoto zake

fifa 17 coins alisema, tarehe 2016-08-08 04:02:06:
Come on, cut it out!
fifa 17 coins http://fifavipnews.weebly.com/home/the-origin-of-fifa-tricks-and-skills

cheapest albion online silver for sale on upalbion alisema, tarehe 2016-08-11 09:03:09:
You did a good job .
cheapest albion online silver for sale on upalbion http://www.upalbion.com/albion/albion-online-silver

U4NBA alisema, tarehe 2016-08-11 13:18:03:
I've been through this!
U4NBA https://www.linkedin.com/in/u4nba

Gasper Gadnce alisema, tarehe 2016-08-20 04:45:31:
This site hatareee sanaaa

wvexbqej alisema, tarehe 2017-01-18 14:38:42:
1

alynwtip alisema, tarehe 2017-01-18 14:38:43:
1

nyyrbbfp alisema, tarehe 2017-01-18 14:38:45:
1

wopledgg alisema, tarehe 2017-01-18 14:38:47:
1

rrmtdgyi alisema, tarehe 2017-01-18 14:38:48:
1

xmnycqak alisema, tarehe 2017-01-18 14:38:50:
1

srxtofwo alisema, tarehe 2017-01-18 14:38:51:
1

textile testing instruments alisema, tarehe 2017-02-20 17:34:38:
i like this site a lot!
textile testing instruments http://wiki.dong-ne.kr/index.php?title=User:LavoieWitcher876

Steven Richard alisema, tarehe 2017-04-16 12:38:34:
Iko poa sana


Albion Online Gold alisema, tarehe 2017-05-10 23:47:39:
I'll be there for you .
Albion Online Gold http://albion.blogghy.com/note/1293235/buy-cheap-albion-online-gold-exclusively.html

textile testing instruments suppliers alisema, tarehe 2017-05-12 10:55:30:
I'm all yours´╝ü
textile testing instruments suppliers http://wiki.fabnews.ru/index.php?title=Textile_Testing_Methods_-_A_Wet_Processing_Industry_Requirement6227705

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
Bookmark and Share
deSiGned by sundo