Aliyekuwa waziri wa fedha wa Lebanon Mohamad Chatah ameuawa kwa bomu mjini Beirut
imewekwa na admin
muda 2014-03-19 11:07:52
Watazamaji 898
Aliyekuwa waziri wa fedha wa Lebanon Mohamad Chatah ameuawa kwa bomu mjini Beirut
Uko hapa : Home > Habari kuu>

Aliyekuwa waziri wa fedha wa Lebanon Mohamad Chatah ameuawa kwa bomu mjini Beirut.

Watu wengine wane waliuawa na takriban Watu 50 wamejeruhiwa katika shambulio linalokisiwa kuwa la bomu lililotegwa kwenye gari.

Chatah,muislamu wa jamii ya Sunni alikuwa mshauri wa Waziri mkuu wa zamani Saad Hariri.pia alikua mkosoaji mkubwa wa Rais wa Syria Bashar al-Assad na chama cha Hezbollah kilichokua kikimuunga mkono Assad.

Kumekuwepo na wimbi la mashambulizi Lebanon,yanayohusishwa na jamii ya Sunni na Shia hasa kuhusu mapigano ya Syria.

Saad Hariri alikuwa akishutumu chama cha Hezbollah kufanya mashambulizi nchini humo.

Watu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa Chama cha Hezbollah wanatarajiwa kufikishwa mahakamani majuma matatu yajayo wakishutumiwa kushiriki mauaji ya Baba wa Saad Hariri na aliyekuwa Waziri Mkuu Rafik,waliouawa kwa shambulio la bomu mwezi Februari mwaka 2005.

Chama cha Hezbollah kimekana kuhusika na kifo cha Rafik Hariri.

Unasemaje kuhusu hii?

mussa alisema, tarehe 2015-08-01 08:43:02:
naipenda tabelltz

Deogracias lucas alisema, tarehe 2015-08-12 05:46:56:
ebhna b!g up xana {tabell} na iyo ngoma jamaa yuko poa xana i mean maitendea hak iy video..

RAPHAEL alisema, tarehe 2015-09-01 02:49:03:
FOR NOW TANZANIA GOING UP ON MUSIC ,KEEP IT ON FOR ALL PEOPLE THEY LIKE OUR TALENT ,FOR I CAN SAY NICE SONG AND VIDEO LOVEEEEE ALLL

denis alisema, tarehe 2016-05-08 14:15:24:
amejitahd kaka akaze

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
Bookmark and Share
deSiGned by sundo