Mapigano Makali yanaendelea nchini Sudan Kusini
imewekwa na admin
muda 2014-03-19 11:07:21
Watazamaji 992
Mapigano Makali yanaendelea nchini Sudan Kusini
Uko hapa : Home > Habari kuu>

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini amesema mapigano yangali yanaendelea katika eneo linalozalisha mafuta la Unity licha ya jitihada zinazoendelea kufanywa na viongozi wa nchi za eneo kuzishawishi pande zote mbili zinazopigana zikubali kusitisha vita mara moja. Kanali Philip Aguer amesema leo kuwa vikosi vya jeshi la serikali vimelazimika kujibu mashambulio ya vikosi vitiifu kwa makamu wa rais wa zamani wa nchi hiyo Riek Machar ambaye serikali ya Juba inadai ndiye aliyehusika na jaribio la mapinduzi ya kijeshi la tarehe 15 mwezi huu. Viongozi wa nchi za Mashariki mwa Afrika kupitia jumuiya ya eneo ya IGAD walieleza mwishoni mwa kikao chao kilichofanyika jana mjini Nairobi, Kenya kwamba serikali ya Sudan Kusini ilikuwa imekubali kumaliza uhasama na waasi wanaodhibiti baadhi ya maeneo ya nchi hiyo. Hata hivyo Riek Machar hakualikwa katika kikao hicho na hivyo kutilia shaka uwezekano wa kutekelezeka pendekezo la serikali la kuwa tayari kusitisha vita. Hayo yanajiri katika hali ambayo kundi la kwanza la askari 72 wa kuongeza nguvu wa Umoja wa Mataifa liliwasili huko Sudan Kusini jana huku umoja huo ukionya kwamba hali ingali ya wasiwasi mno licha ya jitihada za kuzishawishi pande mbili za serikali na waasi kusitisha mapigano. Askari zaidi pamoja na vifaa walitazamiwa kuwasili nchini humo hii leo

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
Bookmark and Share
deSiGned by sundo