Rais wa Fifa Sepp Blatter achunguzwa

Rais wa shirikisho la soka duniani Fifa Sepp Blatter anachunguzwa na viongozi wa mashtaka nchini Uswizi.

Ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali imesema Blatter anachunguzwa kwa “tuhuma za kuhusia katika usimamizi mbaya pamoja na  tuhuma za kutumia vibaya pesa”.Bw Blatter amehojiwa na pia ofisi yake ikapekuliwe, afisi hiyo imesema.

Uchunguzi huo unahusu mkataba wa haki za utangazaji wa runinga ambao Blatter alitia saini pamoja na aliyekuwa mkuu wa soka wa eneo la Caribbea Jack Warner mwaka 2005.Bw Blatter pia anatuhumiwa kufanya “malipo yasiyo halali” mwaka 2011 kwa rais wa shirikisho la soka Ulaya Uefa Michel Platini, taarifa ya afisi hiyo imesema.Mwezi Mei, maafisa saba wakuu wa Fifa walikamatwa Zurich kwa tuhuma za ufisadi kutoka kwa maafisa wa mashtaka nchini Marekani.Blatter alishinda uchaguzi wa urais wa Fifa mara ya tano mfululizo Mei 29 lakini, baada ya tuhuma za ufisadi kukumba shirikisho hilo, alitangaza Juni 2 kwamba angejiuzulu.Anatarajiwa kuondoka wadhifa wake wakati wa mkutano mkuu wa Fifa Februari 26.

Unasemaje kuhusu hii?

mussa alisema, tarehe 2015-08-01 08:43:02:
naipenda tabelltz

Deogracias lucas alisema, tarehe 2015-08-12 05:46:56:
ebhna b!g up xana {tabell} na iyo ngoma jamaa yuko poa xana i mean maitendea hak iy video..

RAPHAEL alisema, tarehe 2015-09-01 02:49:03:
FOR NOW TANZANIA GOING UP ON MUSIC ,KEEP IT ON FOR ALL PEOPLE THEY LIKE OUR TALENT ,FOR I CAN SAY NICE SONG AND VIDEO LOVEEEEE ALLL

denis alisema, tarehe 2016-05-08 14:15:24:
amejitahd kaka akaze

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na admin
muda 2015-09-26 05:48:02
Watazamaji 539
Rais wa Fifa Sepp Blatter achunguzwa
Uko hapa : Home > michezo>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo