Miss Tanzania 2016 "Diana Edward" arejea nyumbani.
Pichani kulia ni mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2016 Diana Edward akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuwasili  leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya Dunia. Miss World Beauty Contest 2016.

Miss Tanzania 2016 Diana Edward aliwasili nchini muda wa saa 10 alasiri na Shirika la ndege la Emirates, na kulakiwa na Waandishi wa Habari, Wazazi wake, baba na mama mzazi, wadau, pamoja na wajumbe wa Kamati ya Miss Tanzania. 
Uongozi wa Kampuni ya Lino International Agency Limited utatoa ratiba ya shughuli zake za kijamii hapo baadae, baada ya mapumziko ya mwisho wa mwaka. 

Tunawatakia Heri na Baraka za Sikukuu ya X Mass pamoja na Mwaka mpya wa 2017.
Mrembo wa Taifa Miss Tanzania 2016 Diana Edward akilakiwa na wazazi wake mara baada ya kuwasili  leo (21 Desemba 2016) akitokea Washington DC Marekani, ambapo alikwenda kushindana katika mashindano ya urembo ya Dunia. Miss World Beauty Contest 2016.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na Kibonde
muda 2016-12-21 13:06:49
Watazamaji 53
Miss Tanzania 2016 "Diana Edward" arejea nyumbani.
Uko hapa : Home > michezo>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo