FARID Mussa Aliyechukuliwa na Timu nchini Hispania Anatupa Kinachoendelea


Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Farid Musa amepost ujumbe kwenye account yake ya Insagram (farid_mussa17) akieleza hali ilivyo baada ya kuwasili kwenye klabu yake mpya ya Tenerife ya Hispania.

Farid aliondoka Bongo usiku wa December 28 kuanza safari ya kuelekea Hispania kujiunga na Tenerife baada ya kusubiri kwa muda mrefu kibali cha kufanya kazi nchini huko ambacho mchakato wake ulichukua muda mrefu hadi kukamilika.

“Thanks God nimeanza mazoezi leo na timu yangu mpya wameshanifanyia medical test ninachosubiri sasa ni leseni kutoka chama chao cha mpira cha Spain.”

“Nimeanza maoezi na timu ya U-23 kwa sababu wanajaribu kunifundisha mfumo wanaoutumia kucheza mechi mbalimbali za U-23 huku nikisubiri leseni yangu, kikubwa kwangu namuomba Mungu aendelee kunipa moyo wa subra nina imani kila kitu kitakuwa sawa.”

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na Kibonde
muda 2017-01-04 01:13:33
Watazamaji 116
FARID Mussa Aliyechukuliwa na Timu nchini Hispania Anatupa Kinachoendelea
Uko hapa : Home > michezo>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo