Picha: Arsenal yatambulisha ndege mpya ya kifahari


Arsenal imetambulisha ndege mpya ambayo itakuwa inaitumia kusafiria kwenda kwenye mechi zake za ugenini za Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ndege hiyo ni ya kifahari na ina kila kitu kinachohitajika ndani. Klabu hiyo iliionyesha ndege hiyo kwenye Instagram wiki iliyopita, aina ya Emir­ates Airbus A380 nje ikiwa im­epambwa na picha za mastaa watano wa timu hiyo; Hector Bellerin, Olivier Giroud, Santi Cazorla, Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Ndani ya ndege hiyo, kila mchezaji ana kitanda chake huku wakiwa wamewekewa anasa kibao, zikiwemo chaneli za televisheni 2,500 na kila mchezaji ana TV yake.

Ndani kuna baa ya kisasa yenye vinywaji vya kila aina, vyoo na mabafu lakini pia maz­ingira mazuri ya kukaa.

The Gunners wataipanda ndege hiyo kwa mara ya kwan­za watakaposafiri kuifuata Bayern Munich mwezi ujao. Angalia picha.

Unasemaje kuhusu hii?

yohana paulus magela alisema, tarehe 2015-10-25 02:57:40:
ngoma iko poa na punch line za hatareee admin keep it up sanua ngoma kalikali

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na Kibonde
muda 2017-01-10 01:56:44
Watazamaji 92
Picha: Arsenal yatambulisha ndege mpya ya kifahari
Uko hapa : Home > michezo>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo