Simba SC kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi na Azama Fc

Klabu ya Simba SC imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi, baada ya kuwatoa watani wao wa jadi, Yanga kwa mikwaju ya penalti 4-2 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Golikipa wa Simba Daniel Agyei ndio alikuwa shujaa kwa upande wa Simba hususan katika changamoto ya mikwaju ya penati. Agyei ameokoa penati mbili za Deogratius Munishi na Mwinyi Haji huku yeye akifunga penati yake baada ya Mkude kufunga ya kwanza.

Simba sasa itakutana na Azam FC Ijumaa katika Fainali. Azam imeitoa Taifa Jang’ombe katika mchezo uliotangulia jioni ya leo.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na Kibonde
muda 2017-01-11 00:49:49
Watazamaji 119
Simba SC kucheza fainali ya kombe la Mapinduzi na Azama Fc
Uko hapa : Home > michezo>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo