Kisoka Tanzania iko chini zaidi Afrika mashariki

Licha ya kupanda nafasi nne hadi nambari 136,Tanzania imeorodheshwa ya chini zaidi na shirikisho la soka duniani FIFA katika soka ya Afrika mashariki.

Kulingana na orodha ya FIFA iliotolewa siku ya Alhamisi,Uganda imeorodheshwa ya 75,ikifuatiwa na Rwanda katika nafasi ya 93.

Uganda na Rwanda zimeshuka nafasi 4 na 15 mtawalia.

Burundi nayo imerodheshwa nambari ya 113 ikiwa ya tatu ikifuatiwa na Kenya katika nafasi ya 131 ikiwa nambari 4.

Taifa Stars ya Tanzania ambayo ililazimu sare ya 0-0 dhidi ya timu ya Super Eagles kutoka Nigeria katika mechi za kufuzu kwa kombe la Afrika inashikila nafasi ya 5 na ya mwisho katika Afrika mashariki ikiwa katika nambari 136 duniani.

Kwengineko orodha hiyo mpya inaonyesha kuwa Liberia na Afrika Kusini ndizo zilizofanywa vyema.

Mataifa hayo mawili yameorodheshwa ya 95 baada ya kupanda kwa nafasi 65 na 144 baada ya kupanda kwa nafasi 54 mtawalia.Kulingana na Shrikisho la FIFA,Ujerumani inaongoza ikifuatiwa na Argentina kisha Ubelgiji nafasi ya 3 na Ureno katika nafasi ya nne.

Unasemaje kuhusu hii?

mrishokafir alisema, tarehe 2015-08-13 09:40:07:
Ni blog kali sana na ni mahiri kwa upakuaji wa ngoma, nawapongeza kwa hilo mmeweza,endeleen kukimbiza around in every where to run de world wide

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na admin
muda 2015-10-04 02:31:33
Watazamaji 453
Kisoka Tanzania iko chini zaidi Afrika mashariki
Uko hapa : Home > michezo>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo