Instagram yazindua video ya matangazo ya moja kwa moja

Mtandao wa Instagram ndio mtandao wa huduma ya kijamii wa hivi karibuni kuzindua video za matangazo ya moja kwa moja.Ukifuata nyayo za mtandao wa facebook,unaomiliki Instagram,You Tube pamoja na programu ya moja kwa moja ya Twitter ya Periscope ,Instagram imezindua programu mpya inayoruhusu wateja wake kuweka matangazo ya moja kwa moja wakati wowote.Mtu yeyote anayetazama anaweza kutoa maoni yake kwa kuweka emoji ambazo hujitokeza katika video hiyo ya moja kwa moja.

Instagram yazindua kanda za video ya moja kwa moja

Inaonekana kuwa ya kawaida,lakini kuna tofauti kubwa.Mara tu unapomaliza kuweka matangazo yako hupotea kabisa.Hiyo inamaanisha hutaweza tena kusambaza link ya video yako kwa wanaotazama na hawataweza kuiona tena baada ya matangazo hayo.Katika taarifa ,msemaji wa Instagram alisema kuwa hiyo inalenga kuwafanya wateja kuhisi faraja na kuweza kusambaza chochote wanachotaka kusambaza.Programu hiyo itasambazwa kwa kundi la wateja wa mtandao huo kabla ya kutumika na kila mtu katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Unasemaje kuhusu hii?

mwamwela alisema, tarehe 2015-10-30 22:33:17:
vyama vya upinzani viongeze nguvu hasa vijjini

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na admin
muda 2016-11-24 02:32:02
Watazamaji 192
Instagram yazindua video ya matangazo ya moja kwa moja
Uko hapa : Home > teknolojia>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo