kutana na Shimo lenye joto zaidi duniani

Wanajiolojia wanasema wanakaribia kupata shimo lenye kiwango cha juu zaidi cha joto duniani.Wanachimba katika volkano kusini magharibi mwa Iceland.Wachimbaji hao wamesema kwamba wanapanga kufika kilomita 5 chini ya ardhi, ambapo viwango vya joto vitazidi 500C (932F), katika kipindi cha wiki chache zijazo.

Wanataka kuchukua mvuke kutoka kwa shimo hilo na kuutumia kuzalisha kawi.Mkuu wa mradi huo Asgeir Margeirsson anasema wanatumai watafikia kina ambacho hakuna aliyewahi kufikia."Hilo ndilo lengo letu - matumaini yetu. Hatujawahi kufikia kina hicho awali, hatujawahi kufikia mawe yenye joto kiasi hiki, lakini tuna matumaini."

Mradi huo unatekelezwa katika rasi ya Reykjanes, ambapo volkano ililipuka miaka 700 iliyopita.Mtambo wa kuchimba umekuwa ukichimba saa 24 kila siku tangu Agosti.Kwa sasa wamefika kina cha 4,500m chini ya ardhi, na wanatarajia kufikia kilomita 5 kabla ya mwaka huu kumalizika.

Mitambo ya kuchimba

Mwanajiolojia mkuu Gudmundur Omar Fridleifsson, wa kampuni ya nishati ya HS Orka anasema: "Joto linaendelea kuongezeka, lakini tunaendelea kuchimba kwenye mawe hayo moto. Nikisema mawe moto, narejelea mawe yenye kiwango cha joto cha 400 hadi 500C."

Wakifikia kina cha kilomita 5, wanatarajia kupata mawe yaliyoyeyuka ambayo yamechanganyika na maji.Mchanganyiko huo una kiwango cha juu sana cha nishati.Wanakadiria kwamba wanaweza kupata kiwango cha nishati mara hata 10 zaidi ya kiwango kinachopatikana katika visimo vya kawaida vya kawe ya mvuke

Bw Margeirsson anasema hilo likifanikiwa, basi lina maana kwamba wataweza kuchimba visima vichache na kupata kiwango cha juu sana cha nishati na hivyo kutoharibu mazingira sana kwa kuchimba visima vya kawi ya mvuke.

Mwaka 2009, kundi jingine lilijaribu kuchimba kwenye volkano lakini walipofikia kina cha 2,100m wakakumbana na mawe yaliyoyeyuka na wakashindwa kuendelea.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na admin
muda 2016-12-15 07:32:29
Watazamaji 232
kutana na Shimo lenye joto zaidi duniani
Uko hapa : Home > teknolojia>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo