Roboti mpya inayoweza kufanya mapenzi kama mtu kutengenezwa.

Je ungependelea kushiriki ngono na roboti? ungefunga ndoa na roboti? na Je roboti anaweza kuwa na haki ya kupinga ndoa hiyo?Haya ni baadhi ya maswala machache yanayoulizwa katika mkutano wa pili wa kuwa na mpenzi wa roboti mbali na kushiriki naye ngono katika chuo kikuu cha Goldsmith mjini London baada ya serikali ya Malaysia ambayo ndio iliokuwa taifa la maandalizi ya mkutano huo kuupiga marufuku.

Hatua hiyo imezua utata sio tu kwa mataifa yenye maoni ya Kihafidhina .Hakukuwepo na wawakilishi kutoka kwa sekta ya ngono wala roboti za ngono katika mkutano huo.Kampuni ya Real Dolls inayotengeza wanaserere wa ngono ilidai kwamba itatengeza roboti wa ngono aliye na akili bandia mwaka ujao.

Uzinduzi huo iwapo utafanyika utakuwa ushahidi wa David Levy ambaye amekuwa akitabiri ujio wa roboti zinazofanana na binadamu zenye akili bandia.Alitoa hotuba ya kufunga mkutano huo ambapo alipendekeza utengezaji wa roboti za ngono.''Tuna roboti za urafiki na sasa roboti ambaye anaweza kuwa mpenzi ndio mtindo mpya''.

Katika kipindi cha miaka 10 ijayo, inawezakana kutengeza roboti ambayo watu wataihitaji kama mpenzi, ina upendo, inaaminika, inaheshima na hailalamiki alisema.Wengi watapendelea uhusiano huo wa roboti na huenda wakataka kufunga ndoa nao.Mpango huo wa mpenzi wa aina ya roboti huenda akazua maswali kadhaa ya kimaadili, hususana wakati ambapo sheria italazimika kutambua roboti kama binaadamu.

Unasemaje kuhusu hii?

Kuwa wa kwanza kucoment hapa!

Tafadhali coment hapa

Name:
Email:
Message:
 
 
imewekwa na admin
muda 2016-12-23 04:03:40
Watazamaji 1035
Roboti mpya inayoweza kufanya mapenzi kama mtu kutengenezwa.
Uko hapa : Home > teknolojia>
Bookmark and Share
deSiGned by sundo